KM asifu imani ya wanachi wa Haiti

21 Januari 2010

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon alisifu imani na ustahmilivu wa wananchi wa Haiti kufuatia tetemeko lililosababisha maafa makubwa wiki iliyopita, akisema ana amini kwamba, kwa msaada wa jumuia ya kimataifa wataweza kukabiliana na maafa hayo.

"Wahaiti wamedhihirisha ustahmilivu wao mara nyingi. Wanaonesha kua na ustahmilivu huo huo na nia ya umoja hii leo. Wa Haiti ni watu wenye imani kubwa ya kidini inayohimili na kuleta faraja wakati mgumu kama huu. Nguvu za imani hazina kipimo. Zina tuhamasisha na kutusaidia tunapokabiliana na matatizo. Zinapunguza machungu yetu na kupunguza mzigo wetu."  

Alisema Haiti inahitaji msaada wetu sote. Mkuu wa UM aliongeza kusema kwamba kwa umoja huo tetemeko hilo la ardhi ni tukio moja pekee kubwa la maafa kuukabili.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter