Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkurugenzi Mkuu wa WFP atatembea Haiti

Mkurugenzi Mkuu wa WFP atatembea Haiti

Mkurugenzi mkuu wa idara ya chakula duniani WFP, Josette Sheeran anatarajiwa kuwasili Haiti Alhamisi kutathmini binafsi hali ilivyo kufuatia maafa kutokana na tetemeko la ardhi la wiki iliyopita.

WFP ilianza kugawanya chakula masaa machache tu baada ya kutokea tetemeko na imeanzisha operesheni ya huduma za dharura itakayogharimu dola milioni 279 ili kuweza kuwafikia wahaiti milioni mbili, pamoja na kutoa huduma za mawasiliano na vifaa kusaidia jumuia kamili inayotoa huduma za dharura. Wakati wa ziara yake ya siku mbili, Sheeran atatembelea maeneo yaliyoathirika na tetemeko la ardhi na kukutana na maafisa wa serikali na watumishi wa kimataifa wa huduma za dharura ambao wengi walijeruhiwa na kupoteza makazi yao na bado wanaendelea kufanya kazi mchana na usiku katika hali nzito kabisa.