Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lazima UM kuendelea na jukumu la mazungumzo ya hali ya hewa

Lazima UM kuendelea na jukumu la mazungumzo ya hali ya hewa

Mkurugenzi mkuu wa Idara ya mazingira ya UM Achim Steiner anasema ni lazima kwa majadiliano ya kimataifa juu ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani yabaki chini ya uwongozi wa UM hata ikiwa mkutano wa viongozi wa Copenhagen mwezi Disemba haukufanikiwa kuleta ufumbuzi.

Bw Stiener anasema hakuna hata kundi moja kati ya kundi la mataifa 20 yaani G20,au mataifa makuu yanayozalisha gesi za greenhouse au kundi lolote, lililofanikiwa kufikia makubaliano kabla ya mkutano wa Copenhagen. Mkurugenzi huyo wa UNEP alikua akizungumza na waandishi habari wakati wa mkutano wa mawaziri wa nishati na mazingira wa Umoja wa Ulaya mwishoni mwa wiki.