Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR:Wasomali elfu 60 wakimbia makazi yao

UNHCR:Wasomali elfu 60 wakimbia makazi yao

Idadi ya majeruhi wa ki-somali na wale wanaopoteza makazi yao inaongezeka kutokana na kuendelea kwa mapigano katika wilaya za kati za Somalia.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, mapigano na usalama kwa ujumla umesababisha kiasi ya watu elfu 63 kukimbia makazi yao huko Somalia. Mapigano yanaendelea katika mji mkuu wa Mogadishu ambako, kufuatana na maafisa wa mji huo, mapigano ya mwisho ya mitaani ya tarehe 13 Januari, kati ya wanajeshi wa serekali na wapiganaji wa Al-Shabab na Hisb-ul-Islam yamesababisha vifo vya watu 10 wakiwemo watoto