Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pakistan yazuia ajenda kwenye mkutano wa kupunguza silaha

Pakistan yazuia ajenda kwenye mkutano wa kupunguza silaha

Majadiliano juu ya kupunguza silaha za nukilia duniani hayakuweza kuanza Ijumanne wakati Pakistan ilipozuia kuidhinishwa kwa ratiba ya 2010 ya mkutano wa Umoja wa Mataifa juu ya kupunguza silaha huko Geneva.

Kuidhinishwa kwa ratiba mwanzoni mwa kikao cha kila mwaka ni utaratibu wa kawaida, lakini balozi wa Pakistan, Zamir Akram aliomba ratiba ipanuliwe zaidi ili kuhusisha masuala mawili zaidi. Mkutano huo ambao ni jopo pekee la kimataifa juu ya majadiliano ya kupunguza silaha, ulikwama kwa sehemu kubwa ya mwaka jana, kutokana na mivutano ya utaratibu iliyosababishwa na Pakistan, hiyo ni baada ya kupatikana ufumbuzi wa kukubaliana juu ya mpango wa kazi kutokana na mvutano wa miaka 12.