IOM yapanga kuunda makazi kwa baadhi ya walokoseshwa makazi Haiti
Kukiwa na idadi kubwa kabisa ya watu walopoteza makazi yao kutokana na tetemeko la ardhi huko Haiti na ukosefu wa vifaa kuweza kutawanya msaada wa dharura, mashirika ya kimataifa na serekali zimeanza mipango ya kujenga makazi makubwa ya muda.
Wakati huo huo Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF), imeeleza wasi wasi wake kuhusiana na athari kubwa kwa watoto walokumbwa na tetemeko la ardhi. UNICEF imetoa wito kwa wote wanaohusika na huduma za dharura kuchukua tahadhari kubwa wanapo kabiliana na watoto walonusurika na maafa na bila shaka watakua na athari zaidi baada hali kutulia.