Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ameahidi msaada wa haraka kwa waathiriwa wa Haiti

Ban ameahidi msaada wa haraka kwa waathiriwa wa Haiti

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameahidi kuharakisha msaada mkubwa wa huduma za dharura unaohitajika kusaidia wa Haiti walokumbwa na mtetemeko mkubwa wa ardhi wiki iliyopita.

Bw Ban alitembelea mji mkuu wa Port-au-Prince siku ya Ijumapili kutathmini binafsi juhudi za uwokozi na kueleza uungaji mkono wake kwa wananchi wa Haiti. Mlolongo wa magari ya Katibu Mkuu ulipita katika baadhi ya mita ya mji mkuu ambako majengo yameporomoka na maelfu ya watu wakiwa wanaishi katika makambi yaliyojitokeza katika viwanja mbali mbali, na maeneo yeyote ambako kuna nafasi. Umoja wa Mataifa unaeleza moja kati ya kila wa Haiti watatu wanahitaji msaada na wengine milioni moja hawana makazi. Bw Ban aliwambia wahaiti kwamba msaada ukonjiani. 

"Kwa nchi ndogo kama Haiti haya ni maafa ya tsunami. Haya ni maafa makubwa kabisa na mzozo mkubwa kabisa wa kibinadamu, ambao kiwango chake huwenda tusiwe na habari nacho kwa hivi sasa hasa nje ya mji mkuu. Maafa yatahitaji jibu kubwa kabisa la msaada."

Idadi ya walofariki inakadiriwa kua ni maelfu na maelfu lakini kungali mamia ya watu hawajulikani walipo bado. Bw Ban amesema ataongeza mipango na idara za umoja wa mataifa nchini humo. Wakati huo huo alitoa shukurani kwa jumuia ya kimataifa inayoisadia Haiti, pamoja na kuwashukuru wale wanaofanya kazi bila kupumzika kujaribu kuokoa maisha ya wathiriwa na kuwasilisha huduma kwa wanaohitaji.