Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM unaitaka Uganda kuondowa mswada dhidi ya mapenzi ya jinsia moja

UM unaitaka Uganda kuondowa mswada dhidi ya mapenzi ya jinsia moja

Kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya haki za Binadamu Navi Pillay aliihimiza serekali ya Uganda siku ya Ijumaa kutupilia mbali mswada wa sheria kuhusiana na watu wa jinsia moja wanaopendana, ambao unatarajiwa kufikishwa bungeni mwishoni mwa mwezi Januari.

Alisema mswada huo utaisababisha nchi hiyo kujikuta katika mvutano wa moja kwa moja na viwango vya kimataifa vya haki za binadam vyenye lengo la kuzuia ubaguzi. Bi Pillay alipongeza taarifa za hivi karibuni za rais na mawaziri wake zikidokeza huwenda wakaingilia kati kuzuia mswada huo ulowasilishwa kibinafsi na mbunge ili kupitishwa kua sheria. Hata hivyo waziri wa habari wa Uganda Aggrey Awori amesema kufuatana na katiba ya Uganda, tabia ya watu wa jinsia moja kupendana imepigwa marufuku, hivyo mswada huo unahusiana na utekelezaji wa sheria hiyo.