Jumuia za kikanda lazima yachukuwe jukumu kubwa pamoja na UM kutanzua mizozo

Jumuia za kikanda lazima yachukuwe jukumu kubwa pamoja na UM kutanzua mizozo

Baraza la usalama lilijadili Alhamisi njia mbali mbali za kuimarisha ushirikiano kati ya Umoja wa mataifa na jumuia za kikanda ili kukabiliana na mizozo ya dunia.

Wakati huo huo Katibu Mkuu Ban Ki-moon alitoa wito wa kutumia uwelevu wakati wa kukabiliana na hali mpya ya matatizo yanaozidi kuwa tete kila wakati. Hapatokei mzozo wowote hivi sasa ambao hauhitaji watu mbali mbali kushirikiana katika viwango mbali mbali kutafuta suluhisho alisema Bw Ban wakati wa hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo wa siku mbili kutafakari njia mpya za ushirikiano. Mkutano huo unahudhuriwa na viongozi kutoka jumuia kadhaa za kikanda kutoka Umoja wa Afrika AU na Umoja wa nchi za Kiarabu, hadi Ushirika wa nchi za Magharibi Nato, Umoja wa Mataifa ya Amerika OAS na Umoja wa nchi za kislamu OIC.