Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu ya wahiti hawajulikani waliko, baada ya tetemeko kubwa la ardhi

Maelfu ya wahiti hawajulikani waliko, baada ya tetemeko kubwa la ardhi

Mashirika ya misaada ya dharura kutoka kila pembe ya dunia yalikua yanajitayarisha siku ya Ijumatano kuanzisha msaada maalum kwa ajili ya Haiti kufuatia tetemeko kubwa la ardhi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 200.

Kufuatana na ripoti za vyombo vya habari kitovu cha tetemeko hilo lililokua na nguvu za 7 nukta 0 kwenye kipimo cha Richter kilitokea maili 10 kutoka mji mkuu wa Port-au-Prince na kuporomosha majengo na miundo mbinu ya mawasiliano na umeme katika mji huo maskini wenye wakazi milioni 2.

Walinda amani wa UM wengi wao kutoka Brazil wamekua wakijaribu kuwaokowa watu kutoka vifusi vya jingo la gorofa tano.