Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji wa kiafrika wahamishwa kusini mwa Italia

Wahamiaji wa kiafrika wahamishwa kusini mwa Italia

Mamia ya wahamiaji wa kiafrika walihamishwa kutoka mji wa Rosarno kusini mwa Italia kufuatia ghasia mbaya kabisa za kikabila huko Italia tangu vita vya pili vya Dunia wasema maafisa wa usalama.

Hatua ya kuwahamisha inafuatia siku tatu za mapambano huko Rosarno katika wilaya ya kusini ya Calabrain, yaliyoanza wakati baadhi ya wakazi kuanza kuwashambulia wahamiaji walokua wanajaribu kuzuia ghasia. Takriban watu 53 pamoja na polisi 18 walijeruhiwa, na maafisa wa usalama wamewahamisha zaidi ya watu elfu moja wengi wao wafanyikazi wa muda kutoka Afrika ambao hawana vibali vya kuishi huko Italia.