Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu ya watu waathirika na mafuriko makubwa Kenya: OCHA

Maelfu ya watu waathirika na mafuriko makubwa Kenya: OCHA

Mvua kubwa zilizoendelea kunyesha kwa wiki mbili zilizopita zimesababisha mafuriko makubwa, katika maeneo ya Kaskazini, ya kati na magharibi mwa Kenya, na kuathiri watu wapatao elfu 30.

Shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya limesema watu 21 wamethibishwa kufa kutokana na mafuriko hayo. Katika mkoa wa Turkana kaskazini mwa nchi hiyo watu walioathirika ni elfu 20, na nusu yao wanahitaji malazi. Mafuriko hayo yamezusha hofu ya kulipuka kwa uongonjwa wa kipindupindu.