Skip to main content

Watu 130 wauawa na wapiganaji wa kijadi wakati hofu ikiongezeka Sudan Kusini

Watu 130 wauawa na wapiganaji wa kijadi wakati hofu ikiongezeka Sudan Kusini

Wapiganaji wa kijadi wenye silaha wa kabila la Nuer wamewaua takribani watu 139 kutoka kabila hasimu wao, katika kijiji kimoja kusini mwa Sudan, amesema afisa mmoja wa serikali hii leo.

Duru mbalimbali zimenukuu Gavana wa jimbo la Warrap, Sabino Makan akisema, "Wamewaua watu 139 na kujeruhi wengine 54. Hakuna yeyote anayejua idadi ya waliokufa kutoka upande wa washambuliaji. Lakini inaweza kuwa kubwa kwa sababu watu wengi walikuja kupigana."