Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Masharika ya misaada yataka dunia kuchukua hatua kuzuia vita mpya Sudan

Masharika ya misaada yataka dunia kuchukua hatua kuzuia vita mpya Sudan

Vita kubwa huenda ikarejea Sudan Kusini iwapo dunia haitachukua hatua ya kulinda mkataba wa amani ambao ulimaliza moja ya vita kubwa na ya muda mrefu barani Afrika.

Onyo hilo limetolewa leo na mahirika kumi ya misaada. Katika ripoti mpya iitwayo "Kuokoa amani ya kusini mwa Sudan, "iliyotolewa katika mkesha wa kumbukumbu ya miaka mitano ya kutiwa saini kwa mkataba huo kati ya serikali ya Sudan na kundi la waasi la " Sudan People's Liberation Movement "(SPLM), mashirika ya misaada yanasema, vuguvugu la ongezeko la machafuko, umasikini uliokithiri, na mvutano wa kisiasa umeuweka mkataba huo katika hatihati ya kuvunjika. Mmoja wa waandishi wa ripoti hiyo Maya Mailer ambaye ni mshauri wa sera wa shirika la Oxfam amesema, "Bado hatujachelewa kuzuia janga hili, lakini miezi kumi na miwili ijayo itakuwa ni mtihani kwa nchi hiyo kubwa kabisa barani Afrika."