Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu imetakiwa kulishughulikia suala la kuwalinda watoto katika vita

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu imetakiwa kulishughulikia suala la kuwalinda watoto katika vita

Mjumbe Maalumu wa KM juu ya Haki za Watoto Walionaswa kwenye Mapigano. Bi Radhika Coomaraswamy, ameitaka mahakama ya kimataifa ya uhalifu kushughulikia suala la jinsi ya kuwalinda watoto wanaojihusisha kwa njia mbalimbali katika vita.

"Watoto mara nyingi wanawajibu mbalimbali katika vita. Hakuna tofauti kati ya wale walio msitari wa mbele katika mapigano na wale wasio husika katika majeshi ya nchini mwao,"Coomaraswamy amesema. "Pia tunataka itambulike bayana kwamba endapo kuna wasiwasi juu ya umri wa mtoto, iwe ni jukumu la yule anayewapa mafunzo kuthibitisha umri wao, iwe ni serikali au makundi mengine. Kauli hiyo ya Bi Coomaraswamy ameitoa wakati wa ushahidi wake katika kesi ya Thomas Lubanga.