Ushahidi dhidi ya Thomas Lubanga kutolewa na mjumbe wa UN

Ushahidi dhidi ya Thomas Lubanga kutolewa na mjumbe wa UN

Mjumbe Maalumu wa KM juu ya Haki za Watoto Walionaswa kwenye Mapigano atatoa ushahidi mbele ya Mahakama ya Kimataifa juu ya Jinai ya Halaiki (ICC) dhidi ya Thomas Lubanga.

Kuanzia tarehe saba ya mwezi huu na kuendelea majaji watasikia ushahidi wa bibi Radhika Coomaraswamy katika kesi ya Thomas Lubanga Dyilo. Atotoa ushahidi huo kutokana na ombi la majaji, wataalamu wa ushahidi na mashahidi wengine watatu ambao ni waathirika. Kufuatia ushahidi wake, kwa wiki ijayo mahakama pia itamsikia Professor Kambayi Bwatshia, ambaye ni mtaalamu wa majina na mikataba mingine ya kijamii katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Na mwisho waathirika watatu nao watapata fursa ya kuelezea mtazamo wao na kutoa ushahidi. Wawili kati yao wataelezea walivyopata mafunzo ya kivita na UPC wakati wakiwa na umri wa chini ya miaka 15 katika eneo la Ituri na wa mwisho atatoa ushahidi wa jinsi watoto walivyokuwa wanaingizwa jeshini Ituri.