UN kusaidia kudadisi mripuko wa volkano Mashariki mwa DRC Congo

5 Januari 2010

Kufuatia kuripuka kwa volkano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani katika JKK (MONUC) unatumia jeshi lake la anga kusaidia kufuatilia kwa karibu kumwagika kwa lava. Volkano ya mlima Nyamulagira uliopo kilometa 40 kaskazini Magharibi mwa Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini iliripuka Jumamosi iliyopita. Ingawa haikumuathiri mtu yeyote lava yake imesambaa kwenye mbuga ya wanayama ya taifa ya Virunga. MONUC imeliweka tayari jeshi lake la anga la India na helikopta, kwa kushirikiana na serikali ya jimbo,wanasayansi wa kituo cha volkano cha Goma, na taasisi ya taifa ya hifadhi ya mali asilli ya Congo (ICCN) kusaidia kutupia jicho shughui za vilkano ya mlima huo. MONUC imesema kwa sasa watu wa Goma , na maeneo yanayowazunguka wako salama, lakini MONUC iko tayari kwa kutoa msaada wa ziada kwa maafisa wa serikali ambao wamewahakikishia wakaazi kuwa volikano ya mlima Nyiragongo haitoathirika na kuripuka kwa volcano ya mlima Nyamulagira.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter