Zimbabwe kufaidika na dola milioni 1.5 ufadhili wa Uholanzi:IOM
Msaada mpya wa dola za Kimarekani milioni 1.5 kutoka serikali ya Uholanzi utasaidia kuchagiza shughuli za kibinadamu za shirika la kimataifa la uhamiaji IOM nchini Zimbabwe kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Msaada huo utalenga kuendelea kuwasafirisha walio na matatizo, kwa kuwapa msaada wa dharura wa chakula na malazi, wasio na makazi, kuwapa msaada wa kuwawezesha kuishi, na kusaidia kuwawezesha kurejea katika maisha ya kawaida haraka iwezekanavyo. Pia utasaidia kufadhili kliniki za dharura ambazo zitatoa huduma za afya bure na kuwawezesha walengwa kupata dawa maeneo ya mijini na viungo vyake. Mfumo wa maji na usafi nchini humo uliathirika vibaya baada ya kuzuka kipindupindu mwaka jana.