Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi kubwa ya watoto njiti wanazaliwa Afriks na Asia:Yasema WHO

Idadi kubwa ya watoto njiti wanazaliwa Afriks na Asia:Yasema WHO

Kuna tufauti kubwa kati ya nchi zilizoendelea na zinazoendelea katika fursa ya kuishi watoto wanaozaliwa kabla ya siku kutimia au njiti.. Takribani watoto njiti milioni 13 wanazaliwa kila mwaka duniani kote, hii ni kwa mujibu kwa takwimu za shirika la afya duniani WHO zilizochapishwa jumatatu.

Na takribani watoto milioni 11 kati ya hao wanazaliwa Afrika na Asia ambao wengi wao hawapati huduma inayotakiwa, amesema mwandishi mkuu wa ripoti hiyo Dktr. Lale kutoka idara ya uzazi salama na utafiti wa WHO, "Mtoto wa wiki 32 anayezaliwa katika nchi zinazoendelea akiwa na uzito wa gram 2000 ana nafasi ndogo sana ya kuishi wakati katika nchi zilizoendelea mtoto aliyezaliwa akiwa na wiki hizohizo 32 ana nafasi sawa ya kuishi kama yule aliyezaliwa kwa wakati muafaka."