Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe Maalamu wa Umoja wa Mataifa ameitaka Sudan kujitahidi kupata utulivu na amani mwaka huu wa 2010

Mjumbe Maalamu wa Umoja wa Mataifa ameitaka Sudan kujitahidi kupata utulivu na amani mwaka huu wa 2010

Mjumbe maalumu wa umoja wa mataifa nchini Sudan, Ashraf Qazi amewatolea wito watu wote wa Sudan kushikamana kutafuta amani zaidi 2010.

Katika salamu maalumu za mwaka mpya Qazi, amesema mwaka 2010 utakuwa muhimu sana kwa mkataba wa amani wa (CPA), uliotiwa saini mwaka 2005 na pande mbili zinazohusika na mgogoro wa Sudan yaani Kaskazini na Kusini. "Kwa kadri itakavyowezekana kila mmoja nchini Sudan anapaswa kufanya kila juhudi aidha kila mtu peke yake au kwa pamoja , kuchangia mafanikio ya  CPA, ambayo yatapimwa kutokana na yakakavyoleta na kuchangia amani ya kudumu," amesema Bwana. Qazi. Na changamoto kubwa ya CPA ni uchaguzi mkuu ujao ambao utakuwa ni wa kwanza wa kidemokrasia utakaojumisha vyama vingi baada ya miongo kadhaa na kura ya maoni ya mwaka 2011ambayo huenda ikasababisha kujitega kwa Sudan Kusini.

.