Skip to main content

Watetezi huru wa haki za binadamu waishtumu Thailand kwa kufukuza nchi watu wa makabila ya Hmong

Watetezi huru wa haki za binadamu waishtumu Thailand kwa kufukuza nchi watu wa makabila ya Hmong

Wataalamu wawili wanaowakilisha mashirika yanayotetea haki za binadamu wametangaza taarifa ya pamoja, iloilaumu vikali Serikali ya Thailand, kwa kuwahamisha kwa nguvu, wahamiaji 4,000 wa makabila ya Hmong na kuwarejesha kwenye taifa jirani la Laos, bila ya idhini yao.

 Wahamiaji hawa wanakhofia watateswa na wenye madaraka wanaporejeshwa Laos. Hatua hii ilichukuliwa na Serikali ya Thailand, licha ya kuwepo upinzani mkubwa kutoka jamii ya kimaaifa. Watetezi wawili hawa wa UM juu ya haki za binadamu, Manfred Nowak, anayehusika na masuala ya mateso na Jorge Bustamante, anayetetea haki za wahamiaji, walitoa taarifa ilioisihi Serikali ya Thailand kusitisha haraka uhamishaji wa kimabavu wa makabila ya Hmong, na kuitaka iwakabidhi wahamiaji wa Hmong yale mashirika ya kimataifa yanayohudumia kidharura wahamiaji, na wakati huo huo kuiomba serikali ya Thailand ihakikishe haki za wahamiaji wa Hmong huwa zinahishimiwa na kutekelezwa kwa kulingana na sheria za kimataifa.