Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO inasema homa ya mafua ya H1N1 imegundiliwa kuenea zaidi Ulaya ya Mashariki kwa sasa

WHO inasema homa ya mafua ya H1N1 imegundiliwa kuenea zaidi Ulaya ya Mashariki kwa sasa

Mataifa ya Ulaya ya kati na mashariki yameripotiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuwa ndio maeneo ya ulimwengu yaliosumbuliwa zaidi sasa hivi na maambukizo ya homa ya mafua.

Taarifa ya WHO imeeleza kwamba wiki chache zilizopita homa ya ILI, aina ya ugonjwa wa homa ya mafua, pamoja na ugonjwa wa kuambukiza mapafu ni maradhi yaliogunduliwa kusambaa zaidi kwenye mataifa ya Georgia, Montenegro na Ukraine, na maradhi ya mapafu yalionekana vile vile kuselelea katika sehemu za Ulaya ya Kusini na Mashariki, hasa katika Ugiriki, Poland, Bulgaria, Serbia, Ukraine na kwenye eneo la Milima ya Urals na katika Shirikisho la Urusi, halkadhalika. Mpaka tarehe 27 Disemba mwaka huu, nchi 208 pamoja na maeneo ya nje kadha mengine kuligunduliwa wagonjwa walioambukizwa homa ya mafua ya H1N1 kwa 2009, maradhi ambayo yalisababisha, kwa ujumla, vifo vya wagonjwa 12,220 duniani.