WFP inayashukuru mataifa kwa kusaidia kuhudumia chakula wenye njaa katika 2009

31 Disemba 2009

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) leo limetoa taarifa maalumu, ya shukurani, kwa Mataifa Wanachama katika sehemu zote za dunia, kwa kazi ngumu na misaada waliochangisha katika zile huduma za kupiga vita njaa ulimwenguni mnamo 2009.

Josette Sheeran, Mkurugenzi Mkuu wa WFP alinakiliwa akisema, "kwa mara ya kwanza katika historia ya shughuli za shirika lao, ulimwengu umekabiliwa na watu bilioni moja wanaougua njaa sugu kila siku." Alikumbusha ya kuwa michango ya walimwengu, pamoja na huduma za kitaifa na jamii, ni vitendo vilivyosaidia sana kunusuru maisha ya mamilioni ya umma wa kimataifa uliobanwa na matatizo ya njaa. Alisema mwongo tuliomo kwa hivi sasa, unakamilisha miaka 10 iliopambwa na umwagaji mkubwa wa damu ulimwenguni na kuzusha mateso kadha wa kadha yanayoambatana na uhusiano wa kimataifa. Alikumbusha Sheeran kwamba watumishi kadha wa shirika la WFP nao pia waliuawa mwaka huu wakati wakiongoza zile shughuli muhimu za kiuutu, za kugawa vyakula kwa umma muhitaji.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter