Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNEP itaisaidia Yemen kitaaluma, kwa kupitia mtandao, kudhibiti mazingira nchini

UNEP itaisaidia Yemen kitaaluma, kwa kupitia mtandao, kudhibiti mazingira nchini

Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) limetangaza kuwa litaipatia Yemen fursa ya kupokea makala muhimu za kisayansi, kwa kutumia taratibu za mtandao, ikiwa miongoni mwa miradi ya kujiendeleza na maarifa ya sayansi ya kisasa kwenye nchi zinazoendelea, katika kipindi ambacho mataifa haya huwa yanakabiliwa na matatizo kadha wa kadha, yanayozushwa na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.