"Ukomeshaji wa janga la H1N1 ulimwenguni huenda ukachukua mwaka", ameonya Mkuu wa WHO

29 Disemba 2009

Dktr Margaret Chan, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), kwenye mahojiano mjini Geneva na gazeti la Le Temps, Ijumanne alinakiliwa akisema janga la homa ya mafua ya H1N1 halitofanikiwa kudhibitiwa kikamilifu mpaka mwaka 2011.

Alihadharisha kwamba walimwengu wanawajibika, katika kipindi cha miezi sita hadi 12 ijayo, kuwa waangalifu na kuchunguza kwa ukaribu zaidi mabadiliko ya maradhi, kabla ya kutangaza ushindi dhidi ya homa ya H1N1. Alisisitiza kusema ni mapema, kwa hivi sasa, kwa WHO kuripoti mafanikio kamili katika kukomesha maambukizi ya homa ya mafua ya H1N1 katika ulimwengu. Alikumbusha ya kuwa muda mrefu umesalia bado kabla ya majira ya baridi kumalizika duniani, na ulimwengu unakabiliwa vile vile na hatari nyengine ya kuripuka janga tofauti la virusi vya homa ya ndege ya H5N1. Kwa hivyo alisema Dktr Chang , tutahitajia mchango wa pamoja kukabiliana na uwezekano wa maradhi haya kuripuka tena kimataifa na kusumbua walimwengu.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter