Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hekaheka za Mkutano wa COP15 zazingatiwa na mtaalamu wa kimazingira kutoka Tanzania

Hekaheka za Mkutano wa COP15 zazingatiwa na mtaalamu wa kimazingira kutoka Tanzania

Majadiliano ya Mkutano Mkuu wa Copenhagen, au Mkutano wa COP15, uliofanyika mwezi Disemba, na yaliochukua wiki mbili, yalipambwa na michuano, mivutano na mabishano yasiotarajiwa juu ya itifaki ya kuzingatiwa na wajumbe wa kimataifa, ili kuimarisha kipamoja Mkataba wa Kyoto, na kuyasaidia Mataifa Wanachama kuwa na chombo cha sheria ya kudhibiti bora athari zinazozalishwa na hali ya hewa ya kigeugeu.

Kwa uchanganuzi kamili wa mtaalamu huyo juu ya Mkutano wa Copenhagen, sikiliza idhaa ya mtandao ya Redio ya UM.