Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtetezi Huru wa Haki za Wafalastina atoa mwito kwa marafiki wa Israel kuishinikiza ikomeshe, halan, vikwazo angamizi dhidi ya umma wa Ghaza

Mtetezi Huru wa Haki za Wafalastina atoa mwito kwa marafiki wa Israel kuishinikiza ikomeshe, halan, vikwazo angamizi dhidi ya umma wa Ghaza

Richard Falk, Mtetezi Maalumu wa UM juu ya Haki za Wafalastina wa Maeneo Yaliokaliwa Kiamabavu na Israel, kwenye taarifa aliotoa kabla ya kumbukumbu ya kutimia mwaka mmoja wa uvamizi wa vikosi vya Israel katika Tarafa ya Ghaza, alisihi mataifa rafiki wa Israel ya Amerika ya Kaskazini na Ulaya kutumia vitisho vya kuweka vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Israel na kuishinikiza ikomeshe vikwazo vyake ilivyouwekea umma wa Ghaza ambavyo vinadhuru wakazi wa eneo hilo kihali na mali. Alisema umma wa kimataifa wenye hisia za kiutu, pamoja na "serikali za dunia na UM, halkadhalika," wanawajibika kuzingatia mateso wanaopitia, na waliopitia, WaFalastina milioni 1.5 wanaoishi kwenye eno la Ghaza, kutokana na vikwazo vya kiuchumi na kijamii vinavyoendelezwa na Israel, na kuzingataia kimakini zaidi ya kuwa nusu ya waathirika wa vikwazo hivyo huwa ni watoto, ambao wanayimwa haki ya kimsingi ya kuishi maisha ya kawaida. Aliitaka Israel ilazimishwe, vile vile, kutekeleza mapendekezo ya Ripoti ya Jaji Goldstone kuhusu ukiukaji wa haki za raia uliofanyika wakati wa mashambulio ya mwaka uliopita dhidi ya raia wa Ghaza.