Mkuu wa UNICEF anajiandaa kumaliza kazi mapema

24 Disemba 2009

KM Ban Ki-moon, ametangaza taarifa ya masikitiko yenye kueleza Ann Veneman, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) kwamba hana azma ya kuendelea kazi tena baada ya muda wake kumalizika.

KM alimpongeza Veneman kwa kutekeleza majukumu yake kwa bidii kubwa, na alisema alihamasishwa sana kutumikia zile huduma za kuwasaidia watoto kuimarisha afya, ilmu na hali njema kote ulimwenguni. Chini ya uongozi wa Ann Veneman, alisema KM, Shirika la UNICEF limehisabiwa kuwa ni kichocheo cha vitendo halisi vya kuwasaidia watoto kutekeleza uwezo wao kamili wa kimaumbile, hasa katika kipindi ambacho UM umepania kukamilisha yale Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya kupunguza, kwa nusu, hali duni, hasa katika nchi zinazoendelea, kabla ya 2015, na kuwasaidia watoto kukabili vyema matatizo yaliojiri kwenye karne ya 21.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter