Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID kujihusisha na huduma za kuwasaidia vijana Sudan kuelewana kwa amani

UNAMID kujihusisha na huduma za kuwasaidia vijana Sudan kuelewana kwa amani

Vikosi vya Mchanganyiko vya UA-UM kwa Darfur (UNAMID) vimeripoti kuwa vitaisaidia Wizara ya Ilmu ya Sudan, kuandaa Mashindano ya 21 ya Taifa, ambapo wanafunzi 7,000 ziada, wanaowakilisha skuli za sekandari za kutoka majimbo 25 ya Sudan hushiriki kwenye mashindano ya kitaaluma na riadha.

Vikosi vya UNAMID vitaisaidia Serikali kwa kuipatia vifaa, mazingira ya usalama na utaratibu wa kudhibiti ugawaji wa vifaa na usafiri. Mashindano haya huwawezesha vijana, kutoka maeneo yote ya Sudan, pia kupata fursa ya kukutana na wenziwao wanaowakilisha makabila mbalimbali, na kufanya urafiki kwa kuendeleza mazungumzo kati yao yatakayosaidia kuondosha zile hisia za kibaguzi na hali ya kutoaminiana miongoni mwao. Mashindano haya yatakayochukua wiki mbili yanatarajiwa kuanza mnamo tarehe 31 Disemba katika El Fasher, mji mkuu wa Darfur Kaskazini.