Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Baraza Kuu Alkhamisi limepitisha bajeti la UM kwa 2010-2011, linalogharamiwa dola bilioni 5.16, hatua iliopongezwa na KM Ban Ki-moon kwa kukamilishwa kwa wakati. Kwa mujibu wa taaarifa iliotolewa kwa waandishi habari, Msemaji wa KM alisema Mkuu wa UM, binafsi, aliahidi "mchango wa bajeti liliopitishwa

na Kamati ya Tano kutumiwa kutekeleza shughuli za UM, utatumiwa kwa umadhubuti na ufanisi wa hali ya juu." KM alitoa shukrani zake kwa uongozi wa Raisi wa kikao cha mwaka huu, cha 64, cha Baraza Kuu, Dr. Ali Treki wa Libya anbaye alihakikisha bajeti lilipitishwa kwa wakati unaofaa. Vile vile KM alipongeza mchango wa Mwenyekiti wa Kamati ya Tano ya Baraza Kuu (Kamati ya Bajeti na Utawala), kwa kuyaongoza majadiliano ya Kamati kwa busara, na aliwashukuru wajumbe wote wa kimataifa walioshiriki kwenye vikao vya mwaka huu vya Baraza Kuu. Mchango wao, alitilia mkazo KM, ulithibitisha kihakika kwamba Mataifa Wanachama yamejifunga kuhakikisha "UM utakuwa kwenye hali njema ya kifedha kuendesha shughuli zake". KM alinakiliwa akisema aliridhika vile vile na maamuzi ya wawakilishi wa kimataifa kuhusu viwango vya malipo ya Mataifa Wanachama kwenye bajeti la UM kwa 2010-2011, na katika kuchangisha bajeti la operesheni za ulinzi amani za UM zinazoendelezwa kwenye sehemu kadha wa kadha za dunia.