Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matukio katika Baraza la Usalama

Matukio katika Baraza la Usalama

Baraza la Usalama asubuhi limepitisha azimio la kuiwekea vikwazo Eritrea. Azimio linapiga marufuku kuiuzia silaha Eritrea au kununua silaha kutoka taifa hili.

Vile vile azimio limeweka vizuizi vya kusafiri, kwa viongozi wa kisiasa na wa kijeshi wa Eritrea, na kuamrisha kuzuia mali zao. Kadhalika, Baraza la Usalama lilipitisha azimio la kuongeza muda wa operesheni za Shirika la UM Kulinda Amani katika JKK (MONUC) ziendelezwe mpaka tarehe 31 Mei 2010, na kumtaka KM awe anafanya mapitio ya mara kwa mara, kuhusu hali ya utulivu nchini kwa ujumla, na juu ya namna MONUC inavyotekeleza majukumu yake. Baada ya hapo mkutano wa Baraza la Usalama ulizingatia hali katika Guinea.