KM amatangaza kuteua naibu mpya wa MONUC kutoka Cote d'Ivoire

KM amatangaza kuteua naibu mpya wa MONUC kutoka Cote d'Ivoire

KM leo ametangaza kumteua Fidele Sarassoro wa Cote d\'Ivoire kuwa Naibu Mjumbe Maalumu wa KM kwa Shirika la UM Kulinda Amani katika JKK (MONUC).

Vile Vile Sarassoro ataitumikia UM kama Mratibu Mkaazi juu ya Misaada ya Kiutu, na atamrithi cheo Ross Mountain wa New Zealand. KM alimshukuru Ross Mountain kwa uongozi wake mzuri na mchango wake wa kiutu, katika kuimarisha shughuli za mashirika ya UM katika JKK. Kuhusu Sarassoro, tangu 2006 alikuwa akiitumikia UM kama Mratibu Mkaazi wa Misaada ya Kiutu na Ofisa Mkazi wa Shirika la UM juu ya Miradi ya Maendeleo (UNDP) katika Ethiopia, ambapo alianzisha utaratibu maalumu, wa kiwango cha juu, uliotumiwa katika huduma za ugawaji wa misaada ya kukidhi mahitaji ya dharura kwa umma waathirika wa matatizo ya kimaumbile na kijamii.