FAO imeripoti 'bei ya chai kwenye soko la kimataifa imevunja rikodi'

22 Disemba 2009

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limechapisha ripoti mpya yenye kuonyesha bei za chai duniani zimefikia kiwango kilichovunja rikodi, kwa mwaka huu.

Lakini inaashiriwa pia kiwango hicho kitateremka mwakani, baada ya majira ya hali ya hewa yatakaporudia utaratibu wa kikawaida, hasa kwenye maeneo yenye kuzalisha, kwa wingi, mazao ya chai, katika mabara ya Asia na Afrika. Bei ya Pamoja ya Chai ya Shirika la FAO, kiashirio kinachotumiwa kupima bei ya chai nyeusi duniani, imekadiriwa mwezi Septemba kufika bei kuu ya dola 3.18 kwa kila kilo moja, katika mazingira yaliopambwa na ukame ulioyavaa mataifa yenye kuzalisha chai ya Bara Hindi, Sri Lanka na Kenya, hali ambayo ndio yenye kuchochea bidhaa ya chai kutakiwa kwa wingi kutosheleza mahitaji ya umma wa kimataifa. Bei wastani ya chai katika mwaka jana ilikuwa ni dola 2.18 kwa kila kilo moja. Shirika la FAO linakhofia kama hali haijadhibitiwa haraka, wakulima wa chai watapata tamaa na kutaka kupandisha chai kwa wingi zaidi, kwa kutegemea bei itaendelea kubakia ya juu, ilhali ukweli wa mambo ni kwamaba soko la chai likifurika mazao hayo, bei itateremka kwa kasi na kuathiri zaidi wakulima wan chi mamsikini, ilisema FAO.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter