Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aweka muda kwa mataifa kutia sahihi Itifaki ya Copenhagen kudhibiti hali ya hewa ya kigeugeu

Ban aweka muda kwa mataifa kutia sahihi Itifaki ya Copenhagen kudhibiti hali ya hewa ya kigeugeu

KM Ban Ki-moon jana alitangaza mwito maalumu kwa mataifa makuu, unaoyanasihi kuongeza bidii zao ili kuhakikisha, katika 2010 kutapatikana maafikiano ya kimataifa yenye sharti kisheria, juu ya udhibiti bora wa mabadiliko ya hali ya hewa katika ulimwengu.

Aliyasema haya kwa sababu ya mizozano iliofumka miongoni mwa Mataifa Wanachama, baada ya kumalizika Mkutano Mkuu wa UM juu ya Athari za Mabadiliko ya Hali ya Hewa, uliofanyika Copenhagen, ambapo nchi wanachama wanaulizana kama Mkutano wa COP 15 ulifanikiwa kutekeleza malengo yake au haukufanikiwa. KM aliyahimiza Mataifa Wanachama kuungana, kimaadili, na kutia sahihi Maafikiano ya Copenhagen ya kupiga vita athari haribifu za mabadiliko ya hali ya hewa. Alipozungumza mbele ya wajumbe wa kimataifa kwenye Baraza Kuu, Ijumatatu ya jana, KM aliahidi kwamba "mnamo miezi ijayo, atajihusisha, yeye binafsi, kwa ukaribu zaidi na viongozi kadha wa dunia ili kuhakikisha kadhia hiyo itakamilishwa" kwa natija ya wote ulimwenguni.