Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya fujo Guinea yakabidhiwa makundi husika na KM

Ripoti ya fujo Guinea yakabidhiwa makundi husika na KM

Msemaji wa KM ameripoti kwamba Ban Ki-moon leo amewatumia makundi kadha husika na tukio la Guinea, ripoti maalumu ya Tume ya Uchunguzi ya Kimataifa juu ya hatua kali za kinidhamu zilizochukuliwa na vikosi vya usalama dhidi ya raia waliokuwa wakiandamana, bila ya fujo, kwenye mji wa Conakry, mnamo mwisho wa mwezi Septemba mwaka huu, ambapo raia wanaokadiriwa 150 waliuawa, na wingi kujeruhiwa.

KM alipendekeza kwa Serikali ya Guinea "kujitenga kabisa na matumizi ya nguvu na mabavu dhidi ya raia" kwa siku za baadaye. Alisema KM kuwa ameshawatumia ripoti ya Tume ya Uchunguzi ya Kimataifawale wote husika, ikijumlisha Serikali ya Guinea, Baraza la Usalama, Umoja wa Afrika (UA) na vile vile kuitumia ripoti Jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi kwa Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS). Tume huru ilioandaa ripoti, ilibuniwa na KM Ban, na ilidhaminiwa jukumu la kuchunguza tukio la tarehe 28 Septemba 2009, pale vikosi vya ulinzi katika Guinea, vilipowadunga risasi waandamanaji raia, kwenye mji mkuu wa Conakry na kuua raia 150, na kujeruhi wingi wa raia wengine wasiohisabika, na vile vile kunajisi kihorera baadhi ya wanawake na watoto wa kike. Baraza la Usalama linajiandaa wiki hii kuzingatia ripoti ya Tume ya Uchunguzi ya Kimataifa kuhusu vurugu la Guinea.