Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OHCHR inasema mashambulio ya LRA Sudan Kusini ni "madhambi yanayokiuka ubinadamu"

OHCHR inasema mashambulio ya LRA Sudan Kusini ni "madhambi yanayokiuka ubinadamu"

Ofisi ya Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu (OHCHR) Ijumatatu imechapisha ripoti mpya juu ya Sudan, ilioeleza ya kwamba mashambulio katili, dhidi ya raia, yalioendelezwa na wapiganaji waasi wa Uganda wa kundi la LRA katika Sudan Kusini, ni vitendo vilivyofananishwa "sawa na makosa ya jinai dhidi ya ubinadamu."

 Ripoti ilibainisha matokeo ya uchunguzi uliofanywa na Ofisi ya UM juu ya Haki za Binadamu na Shirika la Operesheni za Amani za UM Sudan Kusini (UNMIS) kuhusu msururu wa mashambulio 27, yaliothibitishwa kuendelezwa na kundi la LRA, katika kipindi baina ya Disemba 2008 mpaka Machi 2009, ambapo raia 81 waliripotiwa kuuawa, na wingi wengine walijeruhiwa, na walilemazwa, kunajisiwa kimabavu na vile vile kutekwa nyara na wafuasi wa kundi la LRA, ikijumlisha utekaji nyara wa wanawake na watoto 18 waliolazimishwa kushiriki kwenye mapigano wangali na umri mdogo, na pia kufanywa watumwa wa kijinsia, kufanywa wachukuzi na majasusi.