Mtetezi wa Haki za Binadamu Sahara Magharibi aruhusiwa kurejea nchini

Mtetezi wa Haki za Binadamu Sahara Magharibi aruhusiwa kurejea nchini

Taarifa iliotolewa na KM Ban Ki-moon, baada ya saa sita za usiku ya Ijumaa, imeeleza kuwa amefarajika na pia kupata nafuu baada ya kupokea ripoti ilioleza mtetezi wa uhuru wa taifa la Sahara ya Magharibi, Aminatou Haidar, aliruhusiwa kurejea kwao kwenye mji mkuu wa Laayoun.

Hatua hii ilimwezesha Aminatou Haidar kusitisha saumu ya upingaji, iliomchochea kufunga kuanzia kati ya mwezi Novemba, baada ya kunyimwa hali ya kurejea Laayoun, na kulazimishwa kwenda Visiwa vya Kanari, alipokuwa anarejea kutoka Marekani, ambapo alikwenda kupokea tunzo ya mtetezi shupavu wa haki za binadamu. Bi Haidar aliongoza kwa muda mrefu harakati za amani za kugombania haki ya umma wa Sahara Magharibi kujiamulia wenyewe mamlaka, umma unapishi kwenye eneo liliokuwa likitawaliwa na Uspeni na hivi sasa linakaliwa kimabavu na Morocco.