Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya Kamisheni ya Uchunguzi wa vurugu la Septemba katika Guinea imekabidhiwa rasmi KM

Ripoti ya Kamisheni ya Uchunguzi wa vurugu la Septemba katika Guinea imekabidhiwa rasmi KM

KM amekabidhiwa ripoti ya Kamisheni Maalumu ya Uchunguzi ya Kimataifa kuhusu vyanzo vya matukio ya fujo mnamo tarehe 28 Septemba 2009 katika taifa la Afrika Magharibi la Guinea, ambapo raia wapinzani kadha waliripotiwa kuuawa kihorera na vikosi vya ulinzi, kufuatia maandamano yaliofanyika kwenye mji mkuu wa Conakry.

Uchunguzi wa Kamisheni uliendelezwa mjini Conakry kuanzia tarehe 25 Novemba mpaka tarehe 04 Disemba (2009). Hivi sasa KM anafanya mapitio ya ripoti, na anatarajiwa kuwatumia ripoti hiyo, haraka iwezekanavyo, yale makundi husika, ikijumlisha Serikali ya Guinea, Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi kwa Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) na vile vile Baraza la Usalama.