Matumaini yafifia juu ya itifaki ziada kutoka Mkutano wa COP15
Taarifa tulizopokea kutoka Mkutano wa COP15, zinasema matumaini ya kuwakilisha itifaki ziada, kudhibiti bora athari za mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni, yanaanza kufifia,
kwa sababu ya majadiliano kushindwa kufikia maafikiano juu ya masuala ya kupunguza utoaji wa gesi chafu kwenye anga, na kuhusu misaada ya kufadhiliwa nchi maskini ili ziweze kujirekibisha kimaendeleo, hasa ilivyokuwa mataifa haya ndio yanayohatarishwa kudhurika zaidi na matatizo yanayozushwa na hali ya hewa ya kigeugeu.