Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lapitisha maazimio mawili ya Mahakama za Kimataifa na kuhusu Milima ya Jolan

Baraza la Usalama lapitisha maazimio mawili ya Mahakama za Kimataifa na kuhusu Milima ya Jolan

Baraza la Usalama, leo asubuhi, vile vile limeptiisha maazimio matatu, kwa kauli moja. Azimio la awali liliongeza muda wa operesheni za vikosi vya UNDOF kwa miezi sita zaidi,kwenye eneo la Milima ya Jolan, katika Syria, hadi mwisho wa Juni 2010.

Kadhalika Baraza lilipitisha maazimio mawili yanayoruhusu Mahakama ya Kimataifa kwa Iliokuwa Yugoslavia (ICTY) na Mahakama ya Kimataifa juu ya Rwanda (ICTR) kumaliza kusimamia uendeshaji wa kesi ziliosalia, hadi mwisho wa 2012.