Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtetezi wa Haki za Chakula afananisha madhara ya halihewa ya kigeugeu na "bomu liliotegwa dhidi ya udhamini wa chakula"

Mtetezi wa Haki za Chakula afananisha madhara ya halihewa ya kigeugeu na "bomu liliotegwa dhidi ya udhamini wa chakula"

Olivier De Schutter, Mkariri Maalumu wa UM juu ya haki za mtu kupata chakula, amehadharisha Ijumatano mjini Copenhagen ya kwamba sera za kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa, zenye uwezo wa kutekelezwa kwa mafanikio ni zile zinazozingatia kidhati haki za binadamu,

kwa kuhakikisha athari za hali ya hewa ya kigeugeu kwenye mataifa yalio dhaifu kiuchumi na kijamii, zitapunguzwa na kushushwa kwa kima kinachoridhisha. Alinakiliwa akisema "mabadiliko ya hali ya hewa ni bomu la kutegwa linalofuata muda dhidi ya udhamini wa kupata chakula duniani." Alisema inaeleweka madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa, yataathiri zaidi baadhi ya nchi maskini na kusumbua kwa asilimia kubwa raia walio dhaifu kwenye maeneo yao." Aliyahimiza Mataifa Wanachama kuzingatia kilimo kinachosarifika, ili kupambana vyema na matatizo ya njaa na athari za mabadiliko ya hali ya hewa, kwa wakati mmoja."