Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya Malaria Duniani kwa 2009 yachapishwa na WHO

Ripoti ya Malaria Duniani kwa 2009 yachapishwa na WHO

Shirika la Afya Duniani (WHO), leo limetangaza Ripoti ya 2009 juu ya Malaria Duniani. Ripoti ilieleza kwamba muongezeko wa misaada ya fedha, mnamo miaka ya karibuni, kuhudumia malaria, umeyawezesha mataifa kadha kufanikiwa kudhibiti maradhi,

ikijumlisha Eritrea, Rwanda, Sao Tome, Zambia na pia Kisiwa cha Unguja, katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lakini ripoti ilihadharisha pia kwamba miradi ya kudhibiti malaria inahitajia kukuzwa haraka kwa mataifa kuweza kutekeleza kwa wakati lengo la sita la Malengo ya Maendeleo ya Milenia la kupambana na UKIMWI, Malaria na maradhi mengine hatari kwenye maeneo yao.