Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa KM kwa JAK azungumzia hali nchini na wajumbe wa Baraza la Usalama

Mjumbe wa KM kwa JAK azungumzia hali nchini na wajumbe wa Baraza la Usalama

Sahle-Work , Mjumbe Maalumu wa KM kwa Jamhuri ya Afrika ya Kati (JAK), asubuhi aliwasilisha mbele ya wajumbe wa Baraza la Usalama ripoti kuhusu mpango wa amani katika nchi.

Alisema mpango wa amani sasa hivi katika JAK umefikia hatua muhimu sana, inayohusu matayarisho ya uchaguzi wa taifa utakaofanyika mwezi Aprili 2010, kipindi ambacho vile vile mradi wa kupokonya silaha kutoka wapiganaji wa majeshi ya mgambo unatazamiwa kukamilishwa, halkadhalika. Alisema hali, kijumla, katika Jamhuri ya Afrika ya Kati bado ni dhaifu na inahitajia shinikizo la mchanganyiko wa upatanishi unaoridhisha, mchango wa UM utakaotambuliwa na makundi yote kuwa hauna upendeleo, na vile vile kunatakikana msaada wa fedha maridhawa zitakazotumiwa kudumisha amani kote nchini. Baada ya hapo Baraza la Usalama lilizingatia masuala yanayohusu kamati za vikwazo dhidi ya Liberia na Sudan.