Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watumishi wawili wa UNAMID waachiwa huru Darfur

Watumishi wawili wa UNAMID waachiwa huru Darfur

Watumishi wawili wa Shirika la Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID), wanaoitwa Patrick Winful wa kutoka Nigeria pamoja na Pamela Ncube wa Zimbabwe, wameripotiwa kuachiwa huru na hivi sasa wanaelekea makwao.

Watumishi hawa walitekwa nyara na kuwekwa kizuizini na makundi yasiotambulika kwa muda wa siku 107. Kaimu Mjumbe Maalumu wa Pamoja wa UNAMID, Henry Anyidoho, amekaribisha kuachiwa salama kwa watumishi wa UM, na aliishukuru Serikali ya Sudan kwa mchango wake wa kutia kikomo chema tukio hili. Alisema UNAMID itaendelea kutumikia umma wa Darfur kwa lengo halisi la kuimarisha amani ya eneo lao.