UM yathibitisha robo tatu ya vifo vya maafa duniani husababishwa na majanga ya kimaumbile

14 Disemba 2009

Margareta Walhstrom, Mjumbe Maalumu wa KM anayehudumia Mpango wa Kupunguza Athari za Maafa amenakiliwa akisema hali ya hewa mbaya kabisa iliojiri ulimwenguni, katika miezi 11 iliopita, ndio matukio yaliosababisha asilimia 75 ya vifo vinavyoambatana na majanga na maafa ya kimaumbile.

Alisema watu milioni 55 waliathirika na matukio 220 yanayohusikana na hali ya hewa ya kigeugeu, ikijumlisha vifo 7,000 ziada. Alisema mafuriko na dhoruba ni matukio ya kimaumbile yenye kuua kwa wingi watu katika sehemu nyingi za dunia, hasa katika mataifa ya Asia. Kuhusu ukame, alisema ni shida kukusanya takwimu halisi juu ya idadi ya watu wenye kudhurika kihakika na maafa haya. Lakini Wahlstrom alionya ukame ni moja ya janga kuu kabisa lenye kuua watu kwa polepole, kwa sababu ya afya mbaya, matatizo ya utapiamlo na maradhi.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter