Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakati wa kukamilisha itifaki mpya kudhibiti athari za hali ya hewa ni sasa, anasema KM

Wakati wa kukamilisha itifaki mpya kudhibiti athari za hali ya hewa ni sasa, anasema KM

Kwenye mazungumzo na waandishi habari wa kimataifa waliopo Makao Makuu, Ijumatatu asubuhi, KM Ban Ki-moon alitoa mwito maalumu kwa viongozi wa dunia wanaohudhuria Mkutano Mkuu wa UM juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa wa Copenhagen, unaowasihi waongeze, mara mbili zaidi, juhudi zao za

Ban Ki-moon

kuleta masikilizano ya haraka na kufanya muafaka wa kuridhisha kabla mazungumzo ya mkutano kukamilishwa mnamo mwisho wa wiki. Alihadharisha pindi majadiliano yatazorotoa mpaka saa ya mwisho ya mkutano, kuna hatari ya kuwasilisha itifaki isiokuwa na uzito wa kukabiliana kama inavyostahiki athari haribifu na chafuzi zinazoletwa na hali ya hewa ya kigeugeu, isiofuata majira. KM alisisitiza kwenye risala yake kwamba wakati wa vitendo ni hivi sasa, ambapo viongozi wa KiTaifa na serikali 115, ikijumlisha viongozi wanaotoka yale mataifa mawili makuu yenye kuchafua kwa wingi anga, yaani Marekani na Uchina, wamekusanyika pamoja kwenye mji wa Copenhagen kwa matarajio ya kuwa watakamilisha mapatano yatakayosaidia walimwengu kuwakilisha ukuzaji wa uchumi unaosarifika utakaotunza mazingira na kuihifadhi sayari yetu na maangamizi. Alisema watoto na wajukuu wetu hawatopendelea kuachiwa sayari iliojaa sumu yenye kuhatarisha maisha ya walimwengu, kijumla.