Matokeo ya utafiti wa FAO, yathibitisha shughuli za uvuvi ulimwenguni zahitajia marekibisho kudhibiti athari za hali ya hewa ya kigeugeu

12 Disemba 2009

Ripoti ya utafiti ulioendelezwa karibuni na Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO), iliochapishwa leo hii, inaeleza shughuli za uvuvi wa baharini zinakabiliwa na matatizo mbalimbali yanayoambatana na madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa,

na kutokana na uvuvi uliopita kiasi, na vile vile kwa sababu ya kupotea kwa makazi na usimamizi dhaifu wa kuongoza shughuli za uvuvi. Matatizo haya, ilisema ripoti ya FAO, huyanyima mataifa husika uwezo wa kukabiliana vyema na matatizo mapya yanayozushwa na mabadiliko ya hali ya hewa. Mataifa yanayoendelea na visiwa vidogo vidogo - ambayo mara nyingi hutegemea asilimia 50 ya proteini kwa afya kutokana na shughuli za uvuvi na huduma za majini - yanakabiliwa na hatari ya kudhurika kwa urahisi na matatizo haya. Uvuvi wa kwenye mito na kwenye maziwa - ambao hujumlisha asilimia 90 ya shughuli za uvuvi katika mataifa ya Afrika, na Asia - sasa hivi unahatarisha kuwanyima wakazi wa maeneo haya uwezo wa kupata riziki na chakula kwa sababu ya madhara yanayoletwa na mabadiliko ya hali ya hewa. Ongezeko la joto katika maeneo ya Afrika na katika Asia ya kati linabashiriwa kuzidi na kukiuka kiwango cha wastani cha kimataifa, na inaashiriwa tutakapofika 2010 athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa zitashuhudiwa katika asilimia 25 ya mfumo mzima wa ikolojia ya ndani ya nchi barani Afrika.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud