Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waziri Mkuu wa Kenya anazungumzia maendeleo ya uchumi kijani nchini usiochafua mazingira

Waziri Mkuu wa Kenya anazungumzia maendeleo ya uchumi kijani nchini usiochafua mazingira

Wiki hii, mjini Vienna, Shirika la UM juu ya Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) lilifanyisha kikao maalumu kuzingatia uwezekano wa Kufufua Uchumi wa Dunia kwa kutumia Viwanda Kijani, yaani viwanda vitakavyotunza mazingira.

Miongoni mwa wawakilishi waliohudhuria mkusanyiko huu alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kenya, Raila Odinga. Baada ya kumaliza kuhutubia mkutano, Waziri Mkuu Odinga alifanya mahojiano na ofisa wa habari wa UNIDO, Louise Potterton.  Odinga alielezea maoni yake juu ya mada ya mkutano, iliotilia mkazo umuhimu wa kufufua shughuli za kiuchumi kwa utaratibu utakaotumia viwanda vya kijani.

Sikiliza taarifa kamili kwenye idhaa ya mtandao.