Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu ayahimiza mataifa kujikinga na madhara thakili ya ubaguzi

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu ayahimiza mataifa kujikinga na madhara thakili ya ubaguzi

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay, kwenye risala yake kuiadhimisha Siku ya Haki za Binadamu, naye pia alitoa mwito wenye kuzihimiza Serikali na watu binafsi, kote ulimwenguni, kuchukua hatua hakika, na za kudumu, kutokomeza na kukomesha janga la ubaguzi milele duniani.

Alikumbusha kwamba "vituko vya ubaguzi huanza kwa maneno" na alionya kitendo hiki mara nyingi humalizikia kwa mtu kutumia mabavu, ambapo wale wanaotafsiriwa na kubaguliwa kama maadui hupigwa kihorera mitaani, labda kwa sababu ya nguo alizovaa au rangi zao za mwili, na mara nyengine waathirika hawa huteswa kwa mipangilio, na kusababisha makabila yao kumezwa na kusafishwa kutoka jamii zisiowataka, ikijumlisha vile vile makosa ya vita dhidi ya waathirika, na jinai dhidi ya utu, ambayo husababisha mauaji ya halaiki ya makundi yanayodhalilishwa kibaguzi."