Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua ziada zatakikana dhidi ya matumizi ya tumbaku duniani, inahimiza WHO

Hatua ziada zatakikana dhidi ya matumizi ya tumbaku duniani, inahimiza WHO

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza ripoti mpya inayoeleza kwamba licha ya kuwa idadi kubwa ya umma wa kimataifa huhifadhiwa na zile sheria za kupiga marufuku uvutaji sigara kwenye mazingira ya umma, hasa katika 2008, juu ya hayo tumearifiwa kwamba bado tutahitajia kuchukua hatua ziada za dharura, za kuwalinda watu na maradhi pamoja na vifo vinavyoletwa na athari za moshi wa sigara.

Asilimia 94 ya umma wa kimataifa inasemekana hukosa hifadhi inayofaa kutokana na zile kanuni za jumla dhidi ya uvutaji sigara kwenye mazingira ya umma. Taarifa ya WHO, yenye mada inayosema Ripoti juu ya Janga la Matumizi ya Tumbaku Duniani kwa 2009, imeeleza kwamba nchi saba - zikijumlisha Colombia, Djibouti, Guatemala, Mauritius, Panama, Uturuki na Zambia - zimeingiza sheria za jumla, kwenye maeneo yao katika 2008, za kupiga marufuku na kukomesha kuvuta sigara kwenye mazingira yanayotumiwa na umma, hatua ambayo sasa hivi inajumlisha nchi 17 ulimwenguni zenye sheria kama hiyo. Ripoti ilisisitiza matumizi ya tumbaku ni miongoni mwa vitendo vyenye kusababisha vifo vinavyozuilika, hali ambayo inakadiriwa husababisha vifo vya watu milioni 5 kila mwaka.